Shiloleh Achoka kumpigania Zari kwa Diamond
Mwanadada Shiloleh ameonekana kukata tamaa baada ya kukubali kwa shingo upande juu ya mahusiano ya Diamond na mwanamke wake mpya kutoka nchini kenya Tanasha Dona.
Mwanadada huyo ambae kila mara amekuwa akisismama katika majukwaa na waandishi wa habari akisemakuwa mwanamke bora wa kuolewa na Diamond ni Zari ameamua kubwaga anyanga na kuamua kumkubali mwanamke huyo mpya.
Katika moja ya maneno aliyosema shiloleh baada ya kukubaliana na hali halisi alisema “anapopenda kaka yangu sina jinsi, Hi Tanasha , wifi yangu kwa Diamond platiumz na hii ndo Tanzania, karibu wifi yetu nitafanyaje sasa,’
Ikumbukwe kuwa wiki moja nyuma shiloleh alisikia katika uwanja mmoja akisema kuhusu mahusiano hayo huku akitaka Diamond kumuoa Zari na sio Tanasha.