Shilole: Sijaingia Kwenye Ndoa Kwa Ajili Ya Kucheza Mduara
Mwanamuziki wa Bongo fleva Zuwena Ashraf ‘Shilole’ amefunguka na kudai hajaingia kwenye ndoa kucheza mduara yupo kwenye ndoa mazima.
Shilole alizua gumzo wiki iliyopita baada ya kufunga ndoa ya siri na kimya kimya pamoja na mpenzi wake ambaye kwa sasa ni mumewe Uchebe. Ndoa hiyo imezua gumzo Sana kwani ndugu wa Shilole hawakutaka aolewe na Uchebe hadi kufikia hatua ya Shilole kumpeleka Dada yake polisi baada ya kuchukua Simu yake ilimradi tu wazuie harusi hiyo.
Pamoja na misukosuko hiyo Shilole na Uchebe walifunga ndoa ambayo ilihudhuriwa na watu kumi tu. Lakini tangu ndoa hiyo imefungwa Shilole amekuwa mtu wa kulalamika maneno ya kejeli yanayorushwa na watu dhidi ya ndoa yake na Uchebe.
Shilole amefunguka na kusema kuwa watu wasimfikirie ameamua kuingia kwenye ndoa kama maonyesho bali amedhamiria kwenda kuwa mke mwema anayestahili na kuwa mfano wa kuigwa.
Shilole ameongeza kuwa anajua wazi kuwa kuna watu wanamhesabia siku za ndoa yake kuvunjika kama ilivyo kwa mastaa wengine, lakini kwa jinsi alivyodhamiria kutulia kwenye ndoa yake atawashangaza walimwengu.
Najua wazi watu watakuwa wananihesabia siku ndani ya ndoa yangu lakini ukweli ni kwamba nitawashangaza watu wengi na sina sababu ya kuacha kuwa mke bora na mwenye heshima kwa mume wangu kipenzi Uchebe na uhakika Mwenyezi Mungu atatupa miaka mingi”.
.