Shiloleh Na Uchebe Kufunga Ndoa,Honeymoon Ulaya
Mume mtarajiwa wa msanii Shiloleh, mwanadada ambae amekuwa ni moja ya wanawake wapambanaji katika maisha amefunguka na kuongelea mipango yao ya harusi inavyokwenda na jinsi harusi iyo itakavyo fanyika.Mwanaume huyo anaejulikana kwa jina moja la Uchebe amesema kuwa mpiango ya harusi ipo karibuni lakini nia yake kubwa katika harusi hiyo ni kumpeleka mke wake huyo Ulaya kwa ajili ya honeymoon yao.
Akiongea na East Africa, Uchebe amesema kuwa ndoa yao hiyo inategemewa kufungwa mwezi wa kumi na mbili(12) mwaka huu kwa sababu yeye na mkewe mtarajiwa wameshakubaliana kabisa na taratibu za ndoa zimeshaanza kufanyika na wanataka kuhararisha mahusiano yao.
“Mwenyezi Mungu ameshafanya wepesi sasa hivi tupo katika kwenye maandalizi, na Mungu akipenda mwezi wa kumi na mbili itakuwa ndoa kamili kwani taratibu zote nishazifuata,mahari nishatoa sidaiwi kabisa na honey moon nampeleka Ulaya” amesema Uchebe ambae ndie mume mtarajiwa wa Shiloleh
Uchebe ambae sasa hivi ni mume mtarajiwa wa Shiloleh, alishawahi kuwa na ndoa kabla ya hii inayoenda kufungwa sasa, ambapo inasemekana kuwa ndoa hiyo ilivunjika baada ya mwanaume huyo kuingia katika mahusiano na Shiloleh.
Ingwa kwa hivi karibuni pia kulikuwa na tetesi za wawili hao kuwa wameachana baada ya Shiloleh kusema kuwa yeye na vi-ben ten sasa basi, taarifa za kuachana kwao wamezikanusha na kusema bado wanaendelea na mahusiano yao na kwa sasa wapo katika mipango ya harusi.
Mwanadada Shilole ni moja ya wasanii wa kike wenye kupendwa na mashabiki wengi sana lakini pia ni moja ya wasanii wenye ushawishi mkubwa sana kwa mashabiki wake.Ukiachana na kazi ya muziki anayofanya Shiloleh pia ni mama ntilie anaepika chakula mwenyewe na kuwahudumia wateja wake mwenyewe.Amekuwa ni mwanadada anaeangaliwa sana na watu na kuwa mfano wa kuigwa kwa watu wengine.
Ingawa kumekuwa na maneno yanayomkabili kuhusu tabia yake ya kutemba na vijana wenye umri wa chini yake , lakini hajawahi kuathirika na maneno hayo zaidi ya yeye kupiga kazi ili kuwaridhisha masbabiki wake.