Shilole na Uchebe Kufunga Ndoa Hadharani,Hakuna Kadi Ya Mwaliko.
Kwa muda sasa kumekuwa na gumzo mitadaoni kuhusu ndoa ya mwanadada Shiloleh na mumewe mtarajiwa anaejulikaa kwa jina moja la Uchebe. Wiki kadhaa zilizopita Uchebe alithibitisha kufanyika kwa ndoa hiyo mwaka huu mwezi Disemba na kuwa honeymoon atampeleka mke wake huyo mtarajiwa Ulaya.
Nae bibi harusi mtarajiwa amefumnguka na kusema kuwa ni kweli ndoa yao itafungwa hivi karibuni lakini haitakuwa kama ndoa zingine za wasanii ambazo ufanyika kimya kimya.Shilole ameongezea na kusema kuwa katika ndoa yake haitakuwa na kiingilio wala mchango wowote hivyo yoyote anaetaka kuja atakuwa na uhuru wa kuhudhuria na itafanyika mahali peupe bila siri yoyote kama wanavyofanya wengine.
Ndoa yangu sitafanya ya siri kama mabvyo wamekuwa wakifanya wengine,nitafaya sehemu ya wazi kabisaa na wala hata haitakuwa a kiingilio hata kidogo.napenda ndoa yangu ionwe na watu wote na kila mtu aweze kuhudhuria na aoene kila kitu kinachoendelea.
Shiloleh amesema kuwa mpaka sasa ndoa hiyo ina uhakika wa kufanyika na amethibitisha kuwa mwanaume wake tayari ameshatoa mahali kubwa nyumbani kwao na ameshatambulika hivyo mipango ya harusi ndio inafanyika kwa sasa.
Shilole na Uchebe wamekuwa katika mahusiano kwa muda mrefu wa zaidi ya miezi sita sasa ambapo Uchebe aliachana na mke wake wa kwanza wa ndoa kwa kumpa talaka kwa madai ya kuishi na Shiloleh.Hata hivyo wawili hao ambao mpaka sasa wanafanya mpango wa kufunga ndoa wamekuwa wakikumbana na mameno mengi katika mtandao kutokana na mashabiki wa mwanadada huyo kuwa wanamsema anatembea na mwanaume aliye chini ya umri wake.
Shilole ni moja ya wasanii wa kike ambao wamekuwa ni mfano wa kuigwa kupitia kazi anazofanya.Ukiachana na kazi ya muziki anayofanya ambyao ndio ilimtambulisha kwa mashabiki wake, Shiloleh pia aliona fursa ya kufanya biashara ya mama ntilie na ameweza kujitoa kotekote kwa kuwahudumia wateja wake wa chakula na mashabiki zake katika muziki.Hata hivyo Shilole ameweza kumudu majukumu yote kulingana na mahitaji ya watu wake.