Shilole Alamba Dili Nono CRDB
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amelamba Shavu jingine nono Kwenye Kampuni ya CRDB.
Shilole amelamba Dili la ubalozi wa bidhaa mpya kutoka CRDB iitwayo, Sim Account. Kwa sasa watumiaji mbalimbali wa huduma hiyo ya ‘Sim Account’ ya wanajishindia mamilioni ya pesa kupitia promotion mpya ya ‘Shinda na Sim Account’.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5 mara baada ya kutangazwa balozi Shilole amefunguka haya:
Nimefurahi sana kuwa balozi wa Sim Account kwa sababu ni huduma ambayo anaona kabisa inaenda kurahisisha maisha wa watu wa chini, wanavikoba wenzangu, ukitaka kulipa kitu ni rahisi sana na ni huduma ambayo hata mimi mwenyewe nikikaa mbele ya watu wanaweza kujivunia nayo. Kwahiyo nimeaambie tu Watanzania wenzangu na mashabiki wa Shishi, huu ni muda wa kuanza kwenda kidigitali zaidi.
Kwenye biashara yangu ya Shishi Trump Food wateja hawatapata tabu kabisa, ishu za chenji zilikuwa zinasumbua sana lakini sasa hivi kwa Sim Account unaweza kulipa kile unachodaiwa bila usumbufu wa chenji. Pia Sim Account inahuduma mbalimbali ndani yake kama zakulipa bili, wale wenzangu wa vikoba, yaani ni kitu ambacho ukiwa nacho hautapata tabu kabisa kwenye ishu za manunuzi”.
Mwaka huu umezidi kuwa mzuri kwake kwani ameongeza ubalozi mwingine wa CRDB kwani tayari ni Balozi wa kampuni ya simu ya TTCL na British council.