Shilole adai kuwa anatamani kuolewa ila hajapata wa kumuoa
Shilole ambaye ni mmoja wa wasanii maarufu Afrika Mashariki bado hajapata mtu ambaye anaweza kufunga ndoa naye. Iwapo ameonekana na wanaume kadhaa, hakuna ambaye alifika kiwango cha kuwa mume wake.
Hata hivyo, msanii huyu anatamani sana kuoleka kitu ambacho watu wengi hawajui. Akizungumza na Showbiz Xtra hivi karibuni, Shilole alisema kuwa ni wengi ambao wanamtakia mambo mazuri ya ndoa lakini bado anamsubiri yule ambaye mwenyezi mungu atamletea.
Kwa sasa anaamini kuwa siku yake itafika na ataolewa na kuvalia shela (vazi la mwamke siku ya ndoa yake) kama bibi harusi wengine wanavyofanya.
Mrembo huyu alisema,
“Natamani sana na mimi nivae shela ila naamini wakati bado, najua nitavaa tu na watu wataongea sana maana wengine wanajua siwezi kuolewa ila Mungu atanifanyia wepesi na ndoa yangu itakuwa si ya nchi hii,”?|