Shilole Achora Tatoo ya Mwisho Yenye Jina la Mumewe
Mwanamuikzi wa kike ambae pia ni mjasiriamali, Shiloleh ameonyesha tatoo aliyochora kwenye mwili wake yenye jina la mume wake mpendwa uchebe yenye jina ‘ASHRAF‘ na kusema kuwa hiyo ndio tatoo yake ya mwisho kuichora katika mwili wake.
katika ukurasa wake wa instagram , Shilole aliandika”kwa mara ya mwisho nimechora tatooo ya jina la mume wangu nampendaaa sanaaa’
Wasanii wengi wamekuwa na hiyo tabia ya kuchora tatoo zenye majina ya watu wanaowapenda hasa wapenzi wao na kisha kuangaia sana pindi wanapoachana na hii ilishawahi kumkuta Shilole alipochora jina la mpenzi wake wa kwanza Nuh Mziwanda na walipoachana alifuta na kuweka ua, lakini shiloleh amekiri kwa hiyo ndio ya mwisho.