SHILAWADU Wachezea Kipigo Kitakatifu Kutoka Kwa Mose Iyobo

Shirika la Wambe Duniani (SHILAWADU) ni kipindi kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Clouds TV ambacho kinaongelea habari za kimbea kuhusiana na mastaa mbali mbali wa Bongo.

Kipindi hiko kina watangazaji wawili ambao ni Soudy Brown na qwisar. Vijana hao wawili usiku wa Jana walijikuta katika wakati mgumu baada ya kuambulia kipondo kitakatifu kutoka kwa mcheza shoo kutoka WCB Mose Iyobo.

download latest music    

Siku chache zilizopita Tunda na Aunty Ezekiel pamoja na Iyobo waliingia kwenye vita ya maneno baada ya kudaiana chupa ya pombe ya iliyokuwa ina thamani ya tshilingi laki moja. Inadaiwa kuwa Tunda alikopa chupa hiyo na kushindwa kuilipa kwa wakati halo iliyosababisha Aunty Ezekiel kumwashia moto Instagram.

Inadaiwa baada ya sakata hili Shilawadu walifika Dukani kwa Aunty Ezekiel ili wamhoji lakini waliambulia kipigo, Mange Kimambi kaandika taarifa hiyo kama ifuatavyo:

Mose Iyobo kawapa kichapo Shilawadu unaambiwa bonge la ugomvi fujo hapo Dukani kwa Aunty Kinondoni, watu ndio wakaja kuamua na wakashindwa kumhohi Iyobo unaambiwa Qwisar kala vichwa viwili vya kijeshi, Soudy kala mtama double double alikuwa anageukia hewani, basi Shilawadu walijua wanaenda dukani wakamhoji Aunty kumbe yupo China”.

Baada ya sakata hilo time nzmia ya Shilawadu imeachia ujumbe huh kwenye mitando ya kijamii kuhusu kizaazaa hiko;

Kazi yetu ina changamoto kubwa sana, asilimia kubwa ya mastaa wanatuunga mkono, kwa kufanya maamuzi wanayoyataka kulingana na moods wanazokuwa nazo tunapowafata bila kutudhuru. Usiku wa leo tulipokuwa kazini mwagwa damu na mtu tuliyeenda kufanya naye mahojiano kati yetu kuna walioumia mikono, viuno n.k kuna uharibifu wa vifaa vyetu vya kazi umetokea wenzetu wanaendelea na matibabu Mungu ni mwema na hili nalo litapita, bado tuna wasiwasi Kama mhusika atakuwa anaendelea kututafuta atudhuru zaidi. Tunasikitishwa na matumizi makubwa ya nguvu dhidi yetu sisi wanyonge wa Shilawadu”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.