Shamsa Azidi Kuwakaosoa Wanawake Wapenda Ela.
Msanii wa filamu za bongo nchi Shamsa Ford ameendelea kula sahani moja na wanawake wenzie ambao wamekuwa wakipenda kuolewa na wanaume wenye ela bila kujali kuwa maisha siku zote yanatafutwa.hivi karibuni Shamsa Ford aliandika caption ya kumpongeza msanii mwenzie wa kike Shiloleh kwa kuamua kufunga ndoa na mwanaume wake ambae watu walijua hawezi kufunga nae ndoa kutokana na wadhifa mdogo aliokuwa nao mwanaume huyo.
Katika pongezi zake Shamsa Ford hakusita kuwaambia watu hasa wanawake wenzie kuwa ndoa ni uvumilivu na sio kutaka kuolewa na mwanaume mwenye ela bila kujua pa kuzitafuta.Hata hivvo Shamsa alisema kuwa wanawake wengi wamekuwa na tabia ya kusubirI kupewa kila kitu na mwanaume.
Akiongea tena na GPL hivi karibuni, Shamsa Ford anasema kuwa wanawake wengi wamekuwa wakijisahau kuwa sasa hivi maisha yamebadilika , kikubwa ni kuangalia jinsi gani mwanaume uliyenae anakupenda na amekuwa na msimamo na wewe na sio kuwaza kuwa mwanaume mzuri katika maisha ni yule mwenye ela.
Wanawake wengi wamekuwa wanafikiria vibaya kuwa wao wanapaswa kuolewa na wanaume wenye hela tu, na uwezo mkubwa wa kifedha lakini kumbe sio kweli,kikubwa ni kuangalia mwanaume uliyenae anakupenda na amekuwa na msimamao na mapenzi na wewe sio fedha. Alisema Shamsa Ford
Shamsa Ford aliolewa na mwanaume aliyenae sasa hivi mwaka huu , mwanaume ambae ni mfanya biashara wa nguo jijini na Shamsa amekuwa kipaumbele katika kumsaidia mwanaume wake katika biashara hiyo.