Serikali Kuingilia Kati Swala La Mavazi Kwa Wasanii Hasa Wa Kike
Naibu waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na michezo Mh. Juliana Shonza,ametangaza kuwa kuanzia sasa serikali itaanza kazi ya kuwabana wasanii ambao wamekuwa wakivaa vibaya katika kufanya kazi za za kisanii, na kutumia lugha mbaya zikiwemo lugha za matusi katika nyimbo zao.
Mh Juliana Shonza amesema kuwa kwa muda sasa wasanii wamekuwa na mchango mkubwa wa mmomonyoko wa maadili kutokana na nguo mbaya wanazovaa na lugha za matusi wanazotumia katika nyimbo zao.Akiongea alipokuwa akipokelewa ofisini hapo , Naibu Waziri huyo amesema kuwa moja ya vitu alivyoviona katika sanaa ni jinsi wasanii wanavyovaa vibaya katika kazi zao, na ilo ni swala analotaka kuanza kulishughulikia lakini pia lugha mbaya zinazotumika katika nyimbo nalo inabidi kufuatiliwa.
“Nilipoteuliwa swala la kwanza kabisa kuliangalia lilikuwa ni mmomonyoko wa maadili kwakweli imekuwa ni changamoto kubwa sana nimeshuhudia saizi hata ukiangalia kwenye nyimbo na kazi za wasnii lugha ambayo inatumika siyo nzuri,lakini kama haitoshi kuna nyimbo zinaimbwa ukifuatalia kwa ndani unakuta siyo mazuri,lakini hata ktika mavazi nitawaambia wasanii wa kike wajitahidi kuvaa vizuri,kwa sababu hatuwezi kuacha hivi vitu hivihivi vinaendelea tu , kila taifa lina misingi yake na tamaduni zake”
Labda ni kutokana na utandazi na maendeleo yanayoendelea, wasanii hasa wa kike wamekuwa wanavaaa nguo zinazowaacha nusu uchi swala ambalo limekuwa likichangia mmomonyoko wa maadili kwa kiasi kikubwa, na baadhi ya nyimbo zimekuwa na maneno makali ambayo inakuwa vigumu wazazi kusikiliza mbele ya watoto wake.
Lakini pia Naibu Waziri huyo amedai kuwa swala la kuulinda na kuutunza utamaduni wa taifa ni jukumu la viongozi na watu wote kwa ujumla.hivyo basi wasanii wanapofanya kazi pia inabidi kuzingatia kuwa kazi zao zinalenga pia kutunza na kutangaza utamaduni wa taifa lakini pia lugha wanazotumika katika kazi zao zilenge kusikilzwa na watu wa rika zote na sio kubagua kundi fulani, kuna baadhi ya nyimbo zinaweza kuwa na maneno makali kiasi kwamba ni aibu mzazi kusikiliza na mtoto.