Sanchi Azungumzia Swala la Kukodi Ndege Yake
BAADA ya kusemekana kukodi ndege binafsi akitokea Dar kuelekea mkoani Iringa, mwanamitindo maarufu Bongo, Jane Rimoy ‘Sanchi’ amefunguka kuwa hajawahi kukodi ndege zaidi ya kupanda kama abiria wengine.
Akizungumza na Za Motomoto, Sanchi alisema kuwa, alipiga picha tu kama wanavyopiga watu wengine wakishuka kwenye ndege, lakini siyo kwamba alikodi na pia bado hajafikia hiyo hadhi ya kukodi.
“Siwezi kukodi ndege bana, hiyo ilikuwa na abiria wengi tu na mimi nilikuwa ni mmoja wa abiria ila nilipiga picha wakati watu wameshuka ikaonekana nipo peke yangu,” alisema Sanchi.