Sanaa Kumtenganisha koletha Na Mwanae
Akiwa kama mmoja wa wasanii walioanza kufanya kazi za filamu miaka mingi iliyopita Koletha Raymond sasa hivi ameanza kuona kazi ya mikono yake kwa mafanikio aliyoyapata hivi karibuni,mwanadada huyo ambae ameshinda hivi karibuni katika shindano lilikuwa likiendelea la kusaka vipaji vya sauti lilikuwa likiendeshwa nchini ameweza kuwabwaga washiriki wengine na kuweza kushinda nafasi hiyo.
Hata hivyo mshindi wa shindano ilo alipata mkataba wa kufanya kazi nchini China katika mji wa Beijing kwa zaidi ya mwaka mmoja na Koletha ndio amechukua nafasi hiyo , lakini changamoto ilikuwa pale ambapo Koletha anatakiwa kumuacha mtoto wake mdogo mwenye umri kama miezi nane hivi ili aweze kwenda kufaikisha ndoto zake na kuwakilisha tasnia ya filamu Tazania nchini China.
Akijibu kwa ufasaha kabisa kuhusu swala hilo , Koletha anasema kuwa ni kweli ataenda nchini China kufanya kazi hiyo lakini mume wake na familia yake yote ilisha kubali na mtoto atamuacha kwa mama yake mzazi lakini mumewe ameridhia na jambo ilo ilo hivyo anaomba baraka tu kutoka kwao
Mume wangu amenipa ruhusa kwa sababu ni baba muelewa sana,ni mwanaume anaenisaidia katika kila kitu ninachokifanya na tumekuwa tukishikamana sana kwa kila jambo na kwa sasa ameridhika kabisa mimi niende kufanya kazi huko na nitaondoka mtoto nitamwacha kwa mama yangu.nimefurahi sana kwa ushindi huu kwa sababu umenipa fursa ambayo sikuitegemea.-Alithibitisha koletha
Ushindi wa Koletha utasaidia pia kuleta mapinduzi katika tasnia ya filamu ukizingatia kazi yake anaenda kufanyia nchini China hivyo itakuwa pia ni fursa kuitangaza sanaa ya Tanzania mahali pengine kwa sababu huko ataenda na kukutana na watu wengine wenye vipaji pia.Tuanmtakia kila lenye kheri katika kuipeperusha tasnia ya filamu Tanzania na bendera ya Tanzania,tunaamini ataiwakilisha vyema.