Saida Karoli awakanya wasanii wa kike
Msanii wa kike wa bongo fleva kutoka Tanzania ambae kwa muda mrefu alikuwa kimya , lakini sasa amerudi kwa kishindo kikubwa, Saida karoli amefunguka na kuongea na wasanii wenzie wa kike kuacha tabia ya kujikweza na kujidai,kusifia na kujiona wao ndo wao ,na hakuna mtu mwingine zaidi yao,saida amesema kuwa wasanii wa kike ni lazima wawe na discipline katika kazi zao kwa sababu haujui ni nani atakae kusaidia baada ya kuanguka katika kazi na maisha kwa ujumla na kwa ujumla tabia ya kufanya hivyo inakera watu wengi.
Akizungumza na mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha East Africa msanii saida karoli anasema kuwa katika maisha kuna safari ndefu sana ivyo wasanii wanapaswa kuwa makini katika kuongea na kuishi na watu vizuri.
“kwakweli ilo swala ni kero sana, na kero sio kwangu tu bali hata kwa jamii kwa ujumla wake, kwasababu tabia iyo inakufanya unashuka ghafla katika kipaji chako, mtu unapokuwa ma upendo na pia hujisikii na unaongea na watu vizuri wale uliokuwa unaongea nae siku za nyumba ndio hao watakao kusupport n kukubeba pale unapoanguka” ameongea saida karoli . Hata hivyo kwa msanii mkongwe kama Saida Karoli kuongea na kuwaasa wasanii wa kike kuhusu swala ilo inaonyesha kuwa alishaona baadhi ya wasanii hasa wa kike wenye tabia hizo , huu ni muda sasa wa wasanii hao kuanza kubadilika na kuishi vizuri na wasanii wenzao na jamii kwa ujumla
Msanii Saida Karoli ni moja kati ya wasanii wakongwe Tanzania , maarufu sana na alikuwa anatamba na vibao kama chambua kama karanga kipindi cha nyuma kidogo lakini baadae alianguka kimuziki ila sasa amerudi tena kwa kasi na kishindo kikubwa baada ya lebel ya wasafi kumsaini katika lebel iyo na kusimamia kazi zake na sasa hivi anatamba na vibao vyake vipya kama orugambo na kichaka aliomshirikisha gnako na belle 9 na nyimbo izo zinafanya vizuri kila kona