Ruby Aongelea Menejimenti Yake Na Muziki Kwa Ujumla
Msanii wa Bongo Fleva ambae alikuwa ameiteka tasnia ya muziki kwa muda kidogo siku za nyuma ambae pia kipaji chake kimekuzwa kutoka THT, Ruby, amefunguka na kuongelea swala la muziki na maisha yake kwa ujumla.Ruby anasema kuwa kukaa kimya hakuathiri kipaji chake kabisa na wala hakuwezi kufanya kipaji chake kipotee.
Ruby anasema kuwa muziki wa sasa si muziki mzuri tena,wasanii wamekuwa wakifanya muziki biashara hivyo muziki unapotea kabisa.Ruby anakumbuka kuwa alipokuwa akiimba gospel alikuwa akifanya mazoezi wa wenzake kwa pamoja lakini kwa Bongo Fleva kitu icho hakipo badala yake wasanii wa bongo wanajikubali sana.
Alipoulizwa kuhusu menejiment yake Ruby anasema kuwa watu wa mitandao wamekuwa ni watu wa kusema vitu bila kujua ukweli wa kile kinachoongelewa,kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitaja kiwango alichopewa na menejinenti yake ili kufanya tamasha la Fiesta kuwa ni dogo ndio maana yeye akakataa kufanya show iyo na kuwa iyo ndio sababu ya yeye kugombana na menejimenti yake. Ruby anakataa maneno hayo na anasema yeye hakuwahi kuzungumza hivyo, kitu nilichokiongelea kuhusu menejiment yangu ni swala la maslahi,na hata alipoongelea maslahi haikuwa kwamba ni ela ,maslahi ina mambo mengi.
“Sijui kama nilikosea ila kwa kipindi kile ni maamuzi yaliyokuja kwa sababu ya situation ya kipindi kile”anasema Ruby,Ruby anaendelea kusema kuwa endapo atapewa nafasi ya kumwambia Ruge chochote atamwambia tu “nakupenda” kwa sababu ni bosi wake na atabaki kuwa bosi wake.Ruby anamchukulia Ruge kama baba kwa sababu yeye ndie aliemtoa katika muziki na sio bosi wake tu .
“Mimi sina tatizo na Ruge , hata hataa.. kama ningekuwa na shida na Ruge wala hata nisingeongea , watu wanaona nina tatizo na Ruge kutokana na matatizo yaliyotokea, lakini matatizo yanatokea na haina haja ya kujenga bifu na mzazi” anasema Ruby
Ruby anasema kuwa ukipata shida ndio muda wa kuwajua marafiki zako, kuna baadhi ya watu wamekuwa wakimsema kutokana na kusimama kwake kimuziki lakini ukweli ni kwamba ana nyimbo nyingi na anadhani sasa ni muda wa yeye kuzitoa kwa sababu mashabiki wanamuhitaji.