Ruby afunguka sababu za kutemana na Soudy Brown wa Clouds FM
Mrembo na msanii wa bongo Ruby amefunguka kwa mara ya kwanza kudai kuwa hapo awali alitoka kimapenzi na mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown kwa miaka miwili lakini wakaachana.
Kulingana na Ruby aliwachana na Soudy Brown kwa kuwa mtangazaji huyo hakuwa na msimamo. Akiongea kwenye mahojiano Ruby alisema;
“Nikisema nitoke na mastaa wenzangu sio kwamba hawanisumbui wananisumbua sana lakini nawajua tayari the way walivyo. Lakini vitu vingi ambavyo naona wanafanyiwa wasanii wenzangu na mimi kweli nikawe na msanii?
Aliongeza kusema;
”Hapana siwasemi kwa sifa mbaya wasanii lakini mimi siwezi kuisha nao kutokana na tabia zao kwa sababu mimi ni mwepesi sana kuumia. Mimi mwanaume ambaye nimetoka naye kwenye mapenzi na yupo kwenye industry yetu only ni Soudy Brown, na nimeishi naye kwa mwaka mmoja na miezi sita,”
Kuhusu mimba aliyokuwa anasemekana amebeba – Ruby alikana kwa kusema kuwa hajawai kutoa mimba.