Ruby afunguka baada ya kusemekana anatoka kimapenzi na Alikiba
Iwapo hauna habari basi hivi karibuni muimbaji wa Bongo Ruby alisemekana kuwa ndiye mpenzi mpya wa Alikiba. Taarifa hizi zilisabaa kwenye mitandao baada ya wawili hao kuonekana wakiwa pamoja mara kadhaa.
Hata hivyo Ruby ameweza kufunguka kuhusu taarifa hizi na kukana waandishi wanachoandika mitandaoni. Kulingana na Ruby hakuna kinachoendelea kati yake na Kiba huku akiendelea kwa kusema kuwa hata hana namba ya muimbaji huyo.
Hii sio mara ya kwanza Ruby kusingiziwa kuwa anatoka kimapenzi na msanii wa bongo. Hapo mbeleni ilisemekana kuwa alikuwa na uhusiano na Diamond Platnumz hata hivyo sio wengi walioamini.
Akizungumza na Bongo 5 Ruby alisema,
“Na mimi taarifa hizo nimekuwa nikiziona kama wewe ulivyoziona, sioni jipya kwasababu walishawahi kusema kuwa nipo karibu sana na Diamond, sasa wamegeukia kwa Kiba ambaye hata mawasiliano yake sijawahi kuwa nayo.”