Rostam na Maua Sama Wawasanua Mashabiki Zao
Wasanii wa muziki wa Bongo fleva wanaounda kundi la Rostam Roma na Stamina pamoja Maua Sama Wake wateja Mashabiki zao Baada ya kuanzisha msemo wa Tunafunga Jumla jumla.
Katika kurasa zao kwenye mitandao ya kijamii, wawili hao wamekuwa wakiposti picha zao na wakati mwingine wa tukio fulani wakiambatanisha na maneno Tunafunga Jumla Jumla, jambo ambalo mashabiki wengi wamekuwa wakishindwa kung’amua maana yake.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Roma alisema neno hilo alianza kuliona kwa Stamina lakini anashangaa wengine wameanza kuliiga huku wengi wakiomba ufafanuzi.
Ukiniuliza maana yake sielewi ila ni misemo kama ilivyo misemo mingine. Mfano Mangi anaweza kufunga duka akasema nafunga jumla jumla, au mama n’tilie, muuza maji, karanga na wengine wengi kwa hiyo suala la biashara kuna kufunga jumla jumla”.