Rosa Ree- Sipendi Kutongozwa na Mwanaume

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap Rose Robert maarufu kwa jina la usanii kama Rosa Ree amefunguka na kudai kuwa anachukia sana pale inapotokea mwanaume anamtongoza.

Rosa Ree ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘Marathon’ amekaririwa akiiambia Showbiz Extra kuwa kuwa mwanaume akimtongoza hujisikia vibaya na anaweza kumchukia mno, anachohitaji ni kuwa karibu na wanaume kwa ajili ya kazi na kupiga nao stori mbalimbali.

download latest music    

Yaani mwanaume akinitongoza sipendi napenda kama tunakuwa marafiki tu wa muda mrefu kama ikitokea kupendana tutapendana mbele ya safari na si vinginevyo, akinitongoza mapema naona kama ananitamani tu basi alafu animwage”.

Rosa Ree ameshatajwa kuwa na uhusiano na wasanii wenzake kadhaa kama vile Billnas, Young Dee na wengineo ambao wote amedai hana Mahusiano nao na kusema kwa sasa hana mpenzi.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.