Rosa Ree Akanusha Kutoka Kimapenzi na Young Dee
Msanii wa muziki anaefanya vizuri kwenye hip-hop Rosa Ree amefunguka na kukanusha tetesi zinazosambaa kuhusu yeye kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii mwenzie Yound Dee kwa muda sasa.Rosa Ree amesema kuwa watu wamekuwa wakizusha mambo hasa wanapoona watu wamekuwa na ukaribu hata kama ni wa kibiashara na kikazi.
Rosa Ree amefunguka na kusema kuwa kwa muda sasa amekuwa singo bila kujiingiza katika mahusiano yoyote na ikitokea siku akiwa katika mahusinoa yaliyo serious basi lazima atawatambulisha mwanaume lakini sio kupitia katika kurasa za udaku kama inavyotokea saa hivi kwa young dee.
Niko singo siko kwenye mahusiano yoyote yale na mtu yoyote yule,na hata akija mtu na nikawa nae katika mahusiano ntamtambulisha tu kwenu kwa njia proper sio kwa kupitia udaku na sijawahi kutoka na Young Dee ni mwanangu tu nafanya nae kazi na tumekuwa watu wa karibu.
Wasanii wengi wamekuwa wakiambiwa au kuhisiwa kuwa wanatoka na wasanii wenzao lakini wanakuwa wanakanusha lakini ukweli wanaokuwa nao wenyewe na mbaya zaidi mambo yanapokuwa magumu ndio siri zinaanza kuvuja na kushindwa kuyatatua matatizo yao ingawa sio vizuri kuonyesha mahusiano yao katika mitandao.