Rommy Jones Aanika Kilichomvuta Kwa Kay
Kaka na official Dj wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Romeo Jones maarufu kama Rommy Jones amefunguka na kuanika sababu zilizopelekea mpaka kufunga ndoa na mpenzi wake Kijoli au maarufu kama Kay.
Rommy Jones alifunga ndoa na Kay mwaka jana mwishoni baada ya kuwa naye kwenye mahusiano kwa muda mrefu.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Rommy alisema kuwa mkewe huyo alionesha uvumilivu mkubwa enzi za uhusiano wao na ndipo alipobaini kuwa, ndiye mwanamke sahihi wa kumpa heshima ya ndoa.
Niliamua kuoa kwa sababu niliona uvumilivu wa mwanamke huyo kwani nilimfanyia madudu mengi lakini alinivumilia. Kuna wakati nilikua aondoka nyumba na kurudi baada ya siku tatu nikiwa nimelewa lakini alinivumilia, nikabaini huyu ndiye mwenye sifa ya kuwa mke wangu”.