Roma na Pretty Kindy Kurudi Katika Muziki, Diamond Apewa Onyo.
Jana siku ya tarehe 29 March Waziri Mwakyembe alitoa tamko lake kuhusu swala la kufungia wasanii na nyimbo zao na kusema kuwa hakuna msanii yoyote anaechukiwa na basata lakini wanaamua kufanya hayo kwa sababu wanataka muziki wa tanzania kufika mbali zaidi na kwamba wasanii wanapoona wamba wamekosea basi ni bora kurudi BASATA ili kuyazungumza na sio kuanza kuonge katika mitandao.
Kuhusu Diamond, Mwakyemeb amesema kuwa kosa kubwa la Diamond ilikuwa ni kujibizana na Naibu waziri katika mitandao ilhali kulikuwa na uwezekana na kukaa na kuyamzliza.
Akiongezea na kuto habari za furaha kwa mashabiki na wasanii pia , Jh juliana Shonza amesema kuwa waliamua kukaa chini na kupitia maelezo na maombi ya Pretty Kindy ambae pia alifungiwa kwa miezi sita lakini kutokana na mwenendo wake inaonyesha kuwa kuna kitu amejifunza lakini pia ameweza kutimiza yale yote aliokuwa aeambiwa ayafute hivyo wameona kulikio kumpunguzia adhabu kama alivyoomba ni bora kumsamahe kabisa.
Kwa upande wa Roma, Mh Shonza anasema kuwa roma pia aliandika barua kwa baraza ili kuangalia kwa adhabu yake upya nandio baraza lilipoamua kutoa msamaha lakini kukubaliana kuwa nyimbo yake ya kiba100 kutopigwa kwa mfumo wa sauti au video mpaka pale itakapofanyiwa marekebisho yanayotakiwa.
Hata hivyo wasanii hao walipopata nafasi ya kuongea na media kwa upande wa Pretty Kindy anasema anashukuru sana Mungu kwa kutolewa kwaadhabu yake kwa sababu kwa muda uliowekwa ilikuwa ni vigumu sana , nae Roma amewaomba mashabiki na vyombo mbalimbali kutokuuucheza wimbo huo mpaka utakapofanyiwa marekebisho.