Roma Atuhumiwa Kuwa na Urafiki wa Mashaka
Msanii wa muziki wa hip-hop nchini Roma Mkatoliki anadaiwa kuwa mbali na watu ambao alishawahi kufanya nao kazi na kuwa marafiki zake hapo awali.msanii huo anadaiwa kuwatenga na kutokujali urafiki ambao walishawahi kuutengeneza na kuwafaidisha kimuziki.
Msanii Roma anadaiwa kuanzisha urafiki na watu wengi nahata wengine kufanmya nao kazi lakini mwisho wa siku anazinguana nao na kuwatupilia mbali kabisa bila kujali kile walichokitengeneza.Msanii huyo inasemekana alianzisha urafiki na Mose mtambo na kuwa karibu sana lakini baadae walikuja wakazinguana na baadae alikuja kuwa karibuna Dayna Nyange lakini walikuja wakazinguana tena.
Roma pia alikuwa rafiki wa karibu wa msanii Kala Jeremiah ambapo kipindi cha urafiki wao ndipo Roma alikuwa akifunga ndoa, Kala alitoa sapoti kubwa sana katika harusi hiyo lakini kitu cha kushangaza sasa hivi ni kama wamepotezana kabisa ,sasa hivi wako na project na Stamina lakini unakoelekea ni kufa kwa sababu wanazinguana sana.
Hata alipotafutwa kuulizwa kuhusu swala hilo roma alitakia kujibu mashtaka hayo lakini alianza kucheka na kisha kujibu”hizo habari umezitoa wapi, nani kakwambia , sikiliza nikwambie tangu nimeanza musiki huu sijawahi kuzinguana na mwana yoyote kwaio hizo habari hazina ukweli.
Kumekuwa na skendo nyingi sana za wasanii kuwa katika mahusiano ya kirafiki na hata kufanya kazi nyingi nzuri za kufanikiwa pamoja lakini pia bila kujali kuwa urafiki huo unaweza kuwafikisha mbali kimaslahi wanakuja kugombana na kusahau yale waliofanya nyuma.