Reginald Mengi Afunguka Jinsi Jacqueline Alivyookoa Maisha Yake
Mmiliki na Mkurugenzi wa Kampuni ya IPP Reginald Mengi amefunguka jinsi mke wake aliyewahi kuwa Miss Tanzania Mwaka 2000 Jacqueline Ntuyabaliwe alivyookoa maisha yake.
Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha Televisheni cha Citizen cha Kenya, Mzee Mengi amefungukia mahusiano yake na Jacqueline Mengi na kudai kinyume na watu wanavyofikiria haikuwa rahisi kwake kumpata mlimbwende huyo:
Niliwahi kumsikia lakini hatukuwahi kuonana lakini ikatokea nafasi wakati nipo safarini Uingereza ambako nilikuwa na shughuli za kibiashara na Jacqueline alikuwa yuko jijini Birmingham kwenye shughuli zake za muziki”.
Nilitaka kuonana naye wakati yupo Uingereza kwa hiyo nikimualika kuja London kutoka Birmingham huwezi amini hakuja! Lakini nikiendelea kuwasiliana naye kwa simu mara kwa mara lakini hatukukutana lakini tuliporudi Tanzania nilimfukuzia Mpaka alipokubali kwenda matembezi na mimi”.
Mengi amefunguka kuwa baada ya ndoa na kupata watoto mapacha na Mlimbwende huyo, Mengi mwenye miaka 75 anasema kwamba asingekuwa na mrembo huyo labda angekuwa ameshafariki.
Lakini pia Kupitia kitabu chake kinachoelezea maisha yake ‘I can I must I will’ Mengi anazungumzia mrembo huyo Kama mtu aliyeleta mwangaza katika maisha yake.