RC Makonda Atoa Tamko la Jela Kwa Amber Rutty na Atangaza Vita na Mashoga Wote
Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda ametoa tamko rasmi kuhusiana na video cahfu za mrembo Amber Rutty na mpenzi wake lakini pia kuhusiana na ongezeko la mashoga katika jiji la Dar es Salaam.
Kwenye mahojiano na waandishi wa habari, RC Makonda ameweka wazi kuwa Amber Rutty na mpeniz wake wapo lupango muda huu wakati wanasubiriwa kupandishwa kizimbani na kuweka wazi kuwa adhabu yao ni kifungo cha jela;
Tayari yule binti anaitwa Amber Rutty pamoja na bwana yake wapo chini ya polisi tangu kipindi kile nilivyotoa maelekezo na niseme kuwa kosa lile liko wazi na sheria inasema ni aidha kifungo cha maisha au miaka 30 hiyo yote ni kuonyesha ni jinsi gani serikali isivyopendezwa na mienendo inayomomonyoa maadili ya taifa letu”.
Lakini pia Rc Makonda alitangaza vita na mashoga wote ambao wanajihusisha na shughuli za kufanya mapenzi kinyume na maumbile;
Naomba nitoe fursa hii kwa wakazi wa Dar es Salaam namba yangu ya simu inafahamika nimepata taarifa kwamba kuna mashoga wengi sana kwenye mkoa wetu na mashoga hawa ndio kazi yao wanajinadi kwenye mitandao ya kijamii kwaiyo nawaambia wananchi kama kuna shoga yoyote unamfahamu leo mpaka jumapili napokea taarifa za kupatikana kwao”.