RC Makonda Atangaza Kumaliza Bifu na Ruge na Uwepo Wake Fiesta
Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda ametangaza rasmi kumaliza Bifu lake na Mkurugenzi wa Clouds Fm Ruge Mutahaba na kutangaza kushiriki katika tamasha la Fiesta.
Siku ya jana kuna taarifa zilitoka kwamba Ruge Mutahaba anaumwa hoi na hivi sasa yupo nchini South Africa kwa ajili ya matibabu.
Baada ya kuwepo Bifu la siku nyingi kati ya Makonda na Ruge hatimaye RC Makonda ameonekana kuweka tofauti zao pembeni na kuungana na Clouds Fm ili kukamilisha Fiesta.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Clouds Tv, RC Makonda ameelezea mahusiano yake kwa sasa na Boss wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ambapo amesema wamekuwa karibu kama mtu na kaka yake.
Ruge ni kaka yangu, na nikwambie hivyo nilivyompata Keagan (mtoto wa RC makonda) ametunga wimbo maalumu kwa ajili ya Keagan. Unafahamu kama alivyokuwa India (Kwenye matibabu) Mimi nilikuwa na wasiliana nae?. Unafahamu kuwa alishawahi kuja nyumbani kumuona mtoto?. Unafahamu kuwa alishawahi kuja nyumbani kwa ajili ya maombi? Ruge ana watoto… Fiesta nitakuwepo na itakuwa kubwa kuliko”.
Lakini pia Mhe. Paul Makonda amethibitisha kuwa hata yeye atahudhuria kwenye fainali ya Tamasha la Tigo Fiesta, itakayofanyika katika viwanja vya Leaders Jumamosi hii.