RC Makonda Aagiza Harmonize Akamatwe Kama Anavuta Bangi
Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda ameagiza Msanii wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Harmonize Akamatwe kama atakutwa na hatia ya kuvuta bangi.
Makonda ameyasema hayo siku ya jana katika mkutano Wake aliyofanya na wasanii mbali mbali wa Bongo fleva na Bongo Movie ambapo amekemea matumizi ya madawa ya kulevya.
Makonda ameweka wazi kuwa serikali inafanya kazi kubwa ya kupambana na matumizi ya madawa ya kulevya na hivyo haitawavumilia watu ambao watasika kujiingiza huko.
Makonda ameweka wazi anataka Harmonize achunguzwe kama anatumia bhangi kama anavyoonekana kwenye pich zake kwenye Mitandao ya kijamii na kama kweli basi Akamatwe awekwe Ndani.