Ray na Johari Wadaiwa Kuwa Ndani Ya Bifu Zito

Wasanii wakongwe wa filamu za Bongo Movie Blandina Chagula ‘Johari’ na Vincent Kigosi ‘Ray’ wamedaiwa kuwa kwenye bifu zito sana.

Wasanii hao walidaiwa kuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi kwa miaka mingi na hata kumiliki kampuni moja ya kutengeneza filamu ya RJ company ni mahasimu wakubwa hivi sasa.

download latest music    

Global Publishers wanaripoti kuwa Johari na Ray hawaelewani na kudai sababu kubwa ni wivu wa Ray baada ya Johari kupata mpenzi.

Hivi mnajua kuwa Johari na Ray hawana mahusiano mazuri unaambiwa hata kampuni imesambaratika kila mtu anafanya filamu zake lakini Johari muda mwingi yupo mkoani kwa bwana.

Sababu kubwa ya kugombana kwao inadaiwa kuwa Ray amemkasirikia Johari kuwa na bwana mwingine licha ya kuwa yeye ana mzazi mwenzake (Chuchu Hans) lakini bado anamuonea wivu Johari”.

Baada ya Tetesi hizo gazeti la Risasi Jumamosi lilimsaka Ray ili kupata ukweli wa jambo ambapo alifunguka na kukataa kabisa tetesi hizo:

Kuhusiana na kazi mimi najua tunafanya kazi kama kawaida hayo mengine siyajui“.

Lakini pia Johari naye alifunguka:

Kama mimi nina bwana huko Mwanza hata yeye ana mpenzi wake hapa Dar mimi naona hayo mambo si vema kuyaongelea”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.