Ray Kigosi Akiri Kuwa Baba Kumembadilisha Kabisa
Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Ray Vincent Kigosi amefunguka na kuongelea jinsi kuwa baba wa mtoto wake Jayden kulivyombadilisha maisha yake kwani hivi sasa hachelewi kurudi nyumbani kama zamani.
Ray ameelza kuwa tangu awe Baba amekuwa mtu wa kutaka kuwahi kurudi nyumbani ili awe karibu na mtoto wake tofauti na alivyokuwa miaka ya nyumba kabla hajawa Baba.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Amani hivi karibuni, Ray alisema tangu awe mzazi, amejikuta akiwawahi kurudi sana nyumbani na kuacha mambo mengi ya ujana maana anaona ni wakati sasa wa kulea na kumfundisha mwanaye malezi bora.
Daah sasa hivi mimi kabla ya saa mbili lazima niwe nimerudi nyumbani labda itokee bahati mbaya sana. Narudi bwana mwanangu mwenyewe asiponiona tu ni tatizo”:
Jayden ni mtoto wa kwanza wa Ray aliyezaa na Muigizaji mwenzake wa Bongo movie Chuchu Hansy ambaye pia ni mpenzi wake wa siku nyingi.