Rais wa Tanzania atuma pole na salamu za rambirambi kwa familia ziliopoteza wapendwa wao kwa ajali
Rais wa Jamhuri Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewaunga wengi kuwapa pole wazazi na familia ambazo zimewapoteza wapendwa wao baada ya ajali ambayo ilitokea Jumamosi saa 3 asubuhi.
Ajali hiyo ilisababisha vifo vya wanafunzi 32 wa darasa la saba, walimu 2 na dereva wagari la shule ya msingi iitwayo Lucky Vicent ya Arusha. Hii ilitokea baada ya gari waliokuwa wakisafiria kuacha njia eneo la Rhotia Marera na kutumbukia korongoni.
Kulingana na habari inayoenea mitandaoni watu watatu waliepuka na majeruha na kupelekwa hospitali. Rais Magufuli amezitoa rambirambi zake kupitia barua hii.