Rado Amtolea Uvivu Ray Kigosi na Monalisa
Ray na Monalisa wamepata nomination ya tuzo nchi Ghana , lakini baada ya kupostiwa kwa post hiyo kwa ajili ya kuomba kura hakuna aliyekuwa na muhamuko wa kure-post tena kwa ajili ya kuwasapoti wasanii hao wawili , cha ajabu ni kwamba baada ya msanii Ray juzi kuweka kwa mara ya kwanza picha ya mtoto wake wa kiume kwa mara ya kwanza karibia kila msanii aliweza kure-post na kumpongeza msanii huyo kwa mtoto wake huyo.
Baada ya muda maneno yaliendelea kusambaa katika mitandao kwamba kwanini walipoweka post ya kuomba kula hakuna aliewasapoti kwa kuiweka tena katika akaunt zao ili kuwaombea kura kwa mashabiki lakini alipopostiwa mtoto kila mtu akionekana kuvutiwa na picha hiyo na hata kurudia kuipost tena?
Rado, msanii wa muziki na bongo movies pia aliamua kuvunja ukimya na kuwajibu mashabiki lakini pia kutoa ujumbe mkali kwa kuwalipua wasanii hao (Ray na Monalisa) ambao ndio wanawania tuzo hizo nchini Ghana.
Rado ameonekana kukwaza na tabia za wasanii hao wawili ambao ni wakubwa lakini hawana ushirikiano na wasanii wenzao kwa mujibu wa Rado ni kwamba Monalisa na Ray wamekwa hawahudhirii kazi za wasanii wenzao na hata hawatoi sapoti kwa wasanii wenzao,
Kwa kutolea mfano, Rado analalamika kuwa hata kipindi cha uzinduzi wa filamu yake wasanii hao wanaojiita wakubwa na ambao kwa sasa wanataka sapoti walishindwa kuwepo katika uzinduzi wa filamu hiyo.
Kuhusu Ray na Monalisa tunashindwa kusema ukweli kuwa hata wao ni wabinafsi sana,nakumbuka pale Mlimani City nilifanya uzinduzi wa filamu yangu ya Bei kali kati yao wengine wengi hawakuja katika uzinduzi hasa wanaojiita mastaa ingawa walipata kadi ya mwaliko mapema wiki mbili kabla.monalisa alisema anakwenda Zanzibar kutembelea kiwanda na Rich.Niva na Chiko waliamua kulala nyumbani, Ray alimzuia hata mke wake kuja katika uzinduzi.
Kwa muda mrefu wasanii wa bongo movies wamekuwa wakilaumiana wenyewe kwa wenyewe kwa sababu ya kukosa ushirikiano na kujituma katika kukuza tasnia hiyo, ingawa wamekuwa wakikanusha kufa kwa tasnia hiyo Tanzania lakini sanaa ya bongo inaonekana kufa.