Radio Azikwa Kishujaa, Mamia Wajitokeza Kumzika (picha)
Mwanamuziki Mowzey Radio wa nchini Uganda aliyefariki dunia wiki iliyopita February 1, baada ya kulazwa hospitali alipopatiwa matibabu kwa muda wa wiki mbili mfululizo.
Radio alikuwa maarufu kwa kwenye kundi linalojulikana kama ‘Goodlyfe’ na kutoa nyimbo kali kama ‘Bread and butter’. Marehemu alipata majeraha makali baada ya kupigwa kwenye kumbi moja ya starehe.
Mpaka sasa polisi wa mji wa Katwe Uganda wanamshikilia kijana Godfrey Wamala mwenye umri wa miaka 28 ambaye anatuhimiwa uhusika katika shambulio hilo, mpaka hivi sasa Wamala amehamishiwa mjini Entebbe ambapo mtuhumiwa huyo atafunguliwa mashtaka ya mauaji.
Mazishi ya Radio yalifanyika tarehe 3 huko nyumbani kwa mama yake Nakawuka (Kaga) nchini Uganda. Msanii huyo amethibitisha Ushuaia wake kwa jinsi msiba wake ulivyopokelewa na wnanchi wa Uganda kuanzia msiba ulivyotngazwa mamia ya watu walijitokeza hospitalini mpaka kuusindikiza mwili wa marehemu lakini pia mazishi yake yalihudhuriwa na mamia ya watu huku mastaa Chipukeezy na Jaquar kutoka Kenya walihudhuria mazishi.
Hizi ni baadhi ya picha za mazishi ya Radio;