Quick Rocka Afungukia Mahusiano na Kim Nana
Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Aboot Rocka maarufu kama Quick Rocka amefunguka kuhusu mahusiano na mrembo ambaye ni video queen Lilian Kessy maarufu kama Kim Nana.
Kim Nana alijizolea umaarufu miezi michache iliyopita Baada ya kusemekana kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na staa wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz.
Quick Rocka ameibuka na kukana kuwa kwenye mahusiano na mrembo huyo na kusisitiza kuwa mahusiano pekee aliyokuwa naye ni urafiki wa kawaida sana.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Quick Rocka amefunguka haya:
Ni kweli namfahamu Kim Nana kama mtu niliyekuwa nafanya naye kazi tu lakini hakuna mambo ya mapenzi kabisa.”
Tetesi za Kim Nana kutoka na Quick Rocka zilianza baada ya msanii huyo kuonekana anamposti mrembo huyo mara kwa Mara kupitia ukurasa wake wa Instagram.