Queen Darleen Amwaga Povu Kuhusu Mavazi Yake Ya Ajabu
Mwanamuziki kutoka katika label ya WCB na Dada wa Staa wa Diamond Platnumz, Queen Darleen ameibuka na kuwamwagia Povu zito mashabiki ambao wamekuwa wakikosoa mavazi yake.
Queen Darleen amefunguka na kusema nguo anazovaa za kimitego zinazoacha sehemu kubwa ya mwili wake hazina madhara kwake na kwa mpenzi wake.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Darleen Risasi Jumamosi kuwa, mara nyingi anaona watu wanamsema kuhusu nguo anazovaa, lakini hawajui kwamba yeye kama mwanamuziki ndizo nguo anazopaswa kuvaa.
Kinachonishangaza ukivaa kibukta, utasikia watu wanakusema umekaa uchi, sasa sijui wanataka nikiwa ninapanda stejini nivae khanga? Maana hata huyo mpenzi wangu haongei chochote kuhusu mavazi yangu jamani”.
Kwa muda mrefu sasa Queen Darleen amekuwa akikosolewa sana na mashabiki zake kutokana na mavazi yake ya kimtego ambayo amekuwa akivaa na kujianika kwenye mitandao ya kijamii.