Queen Darleen Adai Yeye ni Mkali Wa Mapenzi
Msanii wa muziki wa Bongo fleva na First Lady wa WCB, Queen Darleen ameibuka na kujitamba kuwa yeye ni mkali pale linapokuja Suala la mapenzi hakuna wa kumshinda.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Sam Misago Tv, Queen Darleen alianza kujisifia na kujimwagia sifa kemkem huku akidai kuwa yeye ni mtamu na romantic sana kwenye mapenzi.
Nakwambia Mimi ni mtamu halafu niko romantic sana kwenye Suala la mapenzi.
Halafu pia sinaga historia ya kuwa kwenye mapenzi na mwanaume kwa Wiki mbili wiki tatu halafu akiondokaga lazima tu arudi”.
Lakini pia pamoja na kujimwagia sifa kibao Queen Darleen alifunguka kuhusu mapenzi yake:
Kwenye mahusiano yangu kwanza mtu akinitongoza huwa nachukia sipendi kabisa kutongozwa na isitoshe huwa sisubiri mtu anitongoze maana kunakuwa na uongo mwingi mtu anakwambia anakupenda wakati anakutamani”.
Queen Darleen ameweka wazi kuwa hata yeye akivutiwa na mwanaume na alamtamani lazima apite naye na pia ana uhakika hakuna mwanaume anayeweza kumkataa kwa sababu yeye ni staa na pia Dada yake Diamond.