Professa Jay afunguka kuhusu jumba lake la kifahari kuwekwa alama ya kubomolewa (Picha)
Mbunge wa Mikuni Joseph Haule maarufu kama Professor Jay ni miongoni mwa watu ambao nyumba zao zimewekewa alama ya X kuashiria zipo katika hifadhi ya barabara.
Professor Jay amejenga jumba lake la kifahari pembezoni mwa barabara ya Morogoro maeneo ya Mbezi Luis, jijini Dar es Salaam.
Hivi karibuni Tanroads imetangaza kuwa muda wowote itaanza utekelezaji wa kubomoa nyumba zilizowekewa alama ya X katika barabara hiyo kupisha ujenzi wa barabara kubwa ya kisasa.
Professor Jay amefunguka kuhusu jumba lake kuwekwa alama ya kubomolewa;
“Wanasema kupanua ni meta 121.5 ni upana mkubwa sana na upande mkubwa sana na watu wengi wataarithirika na wataumia. Kwa sababu tunaamini haki inapatikana mahakamani ndio maana tukaenda kuweka zuio, kuangalia ni jinsi gani tunaweza kupata haki yetu ya msingi lakini kitu kikubwa tunachozidi kusisitiza hakuna mtu anayekataa kuhama kwa ajili ya maendeleo.
“Wengine tumejenga kwa muda mrefu sana, nakumbuka hii nyumba nimejenga kupitia muziki, unapata lakini mbili unatoa elfu hamsini unanunua misumari halafu laki na nusu unakula bata, kwa hiyo unapoona kwamba inabomolewa kwa siku moja na hakuna fidia serikali inatakiwa iangalia kwa jicho pevu,” Professor Jay ameimbia XXL ya Clouds FM.