Profesa Jay Kumtembela Lulu Gerezani
Mwanamuziki mkongwe wa bongo hip -hop ProfesaJay anasema kuwa siku yoyote kuanzia sasa yuko mbioni kwenda kumtembelea msanii wa bongo movie lulu michael ambae ayupo gerezani akitumikia kifungo chake cha miaka miwili baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia.
Profesa Jay anasema kuwa anaamini kabisa kuwa lulu ana mengi ya kuongea hivyo anatamani sana kuongea nae ili aweze kumwambia yalitopo moyon mwake na pia kumfariji kwa kila analopitia kwa sasa.
Ninatamani sana kuonana na lulu niweze kuzungumza nae,ninafahamu ana mengi ya kuzungumza na hivyo ninajipanga na muda pia na ikiwa tayari nitawafamisha ni lini ninakwenda kumuona.- Alisema Profesa Jay ambae kwa sasa anafanya vizuri na kibao chake kipya cha Pagamisa alichomshirikisha Mr.T-Touch