Pretty Kindy Agoma Kulinganishwa Na Kina Amber Lulu

Moja wa wasanii wa wanadada mwenye vipaji vingi na amekuwa akifanya vizuri katika  bongo fleva, u-video queen lakini pia ni muigizaji wa  filamu katika bongo movies mwanadada Pretty Kindy amefunguka na kusema kuwa katika kazi ya u-video queen  hakuna wa kulinganishwa na yeye kwa sababu yeye ana kipaji na anajiamini sana na kazi yake.Akiwa ndio anachipukia na kufanya vizuri katika tasnia zote tatu , mwanadada huyo anasema kuwa ukiachana na Amber Lulu na wengine wote yeye ni zaidi ya wote katika kazi hiyo.

Akiongea katika mahojiano na mwandishi wa gazeti moja la  Amani , Pretty Kindy anasema kuwa kwa upande wake hawezi kukimbia na kuacha kazi ya kuwa video queen kwa sababu anaamini kabisa anafanya kazi hiyo vizuri na anategemea kulipwa vizuri kabisa kwaiyo wala hana mpango wa kuitupa kazi hiyo kwa sababu pia inamueweka mjini.Akitolea mfano wa ma-video queen wengine kama Gigy Money na Amber Lulu ambao wanasemekana kuachana na kazi ya kuwa video queen an kujikita zaidi katika kazi ya muziki.

download latest music    

Kwakweli hakuna kitu cha kufanya wanilinganishe na hao wengine,juzi kati nilikula deal nono sana la uvideo queen  katika video ya msanii benny kinyaiya na nililipwa vizuri sana.siwezi kukimbia kazi hii  kisa malipo kwa sababu  kama ni fedha ninajua kabisa nitalipwa pesa zangu  za kutosha kulingana na kazi yangu nzuri  inavyoifanya kwa sababu ninajiamini.-alifunguka mwanadada huyo

Mwanadada huyo amesema hayo baada ya kuona ma-video queen wengi wamekuwa wakikimbia kazi hiyo kutokana na kudai kuwa maslahi ya kazi hiyo imekuwa ni madogo sana, ambapo moja ya watu hao ni Amber Lulu na Gigy Money ambao wameachana na kuwa video queens na kuingia zaidi katika kazi ya kuimba tu.

Mwanadada Pretty Kindy ni moja wa wasanii wa filamu vizuri akiwa amecheza vyema pia katika filamu ya Riyama Ally inayojulikana kama  Damu yangu na ile ya Baba Haji ya Who is back.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.