Post ya Uwoya kwa Msami Yazua Gumzo Mtandaoni
Mke wa msanii Dogo Janja amezua maneno katika mtandao wa instagram baada ya kuweka picha ya mwanaume aliyewahi kuwa nae katika mahusiano kipindi cha nyuma kabla hajaolewa na Dogo Janja na kufanya watu kupigwa na butwaa kwanini kumpost mwanaume huyo na kuandika maneno ambayo yapo kama anamkomoa mtu mwingine.
Katika ukursa wake wa Instagram, Irene aliandika “the best dancer in africa,….usiforce ndio kuwa hapana…and plzzzzzzz panic at your own risk…”
Baada ya hapo msanii mwenzake Steve Nyerere alimuomba Irene aache mchezo aliouanzisha na kumwambia kuwa hawataki kufanya tena vikao vya kusuluisha matatizo yao ya ndoa pindi watakapo gombana.
Lakini pia baadhi ya nao mashabiki hawakuwa nyuma kutoa yao ya moyoni kwa kitendo hicho cha Irene uwoya na kumwambia kuwa kwa sasa ameolewa hivyo aache kupost picha za wanaume wa watu wengine, ingawa pia Irene alionekana kutotaka kupewa ushauri na watu wengine.