Picha Ya Wema Na Bwana Mpya Yazua Utata Kwa Mashabiki
Ikiwa ni kama desturi sasa kwa baadhi ya wasanii kuvujisha picha za siri wakiwa faragha na wapenzi wao , na inaonekana kama ni jambo la kawaida wakati swala la mapenzi ni siri kati ya watu wawili, hivi karibuni zimeibuka picha nyingine zikimuonyesha msanii wa Bongo Movie, malkia wa urembo, kipenzi cha wengi mwenye majina lukuki Wema Sepetu akiwa na mwanaume mpya . Msanii huyo ambae tangu kuwepo kwa picha hizo katika mitandao hajaamua kujibu kitu chochote lakini imekuwa ikileta tafrani kwa baadhi ya mashabiki huku wengine wakimpongezana na kumsifia kuwa na mahusiano huku wengine wakimponda na kumtukana na kumwambia kuwa ni bora hasithubutu kuvujisha picha hizo hadharani.
Msanii huyo ambae pia amepitia mahusiano ya mapenzi na wasanii na watu wengi maarufu katika tasnia ya sanaa hasa katika bongo fleva ikiwepo Diamond Platinumz, TID, Mr.Blue kwa kipindi cha nyuba na hivi karibuni alikuwa akitoka na mshindi wa big brother kutoka Tanzania Idris Sultan haonekani kukoma na tabia ya kuweka mahusiano yake wazi ilhali mahusino yake mengi ya kimapenzi yamekuwa hayadumu kwa muda mrefu.
Wapo baadhi ya washabiki wamekuwa wakisema kuwa picha hiyo ni moja ya sehemu za movie yake mpya ambayo itatoka hivi karibuni, lakini baada ya waandishi wa habari kufatilia na kupata video clip ya picha hiyo ni dhahiri kuwa picha iyo hausiani na utengenezaji wa filamu yoyote ya msanii huyo.Hata hivyo katika video clip iyo kuna baadhi ya maneno yanayosikika Wema Sepetu akiongea huku akiwa kama anamponda moja ya mabwana zake aliowahi kuwa na uhusiano nao wa kimapenzi huko nyuma.
Hata hivyo , hii ina maanisha nini kwa baadhi ya wasanii ni kusema kuwa hawana privacy, au kwa sababu wao ni wasanii basi kila kitu kinakuwa wazi, baadhi ya mashabiki wamekuwa wakiandiak maoni kwa msanii huyo wakimtaka aongele kuhusu picha hizo na atoe uthibitisho wa kile kinachosemwa katika mitandao.Wema ni moja kati wa mastaa wa kike ambao wamekuwa wakisema na kutukanwa sana na mashabiki katika mitandao kwa karibia kila tukio analolifanya , linaweza kuwa zuri au baya.