Picha Tata Za Prezzo na Amber Lulu Zaleta Gumzo
Mwanamuziki Prezzo kutoka Kenya na Video vixen maarufu Bongo Amber Lulu wameingia kwenye skendo nzito mara baada ya picha inayowaonyesha wakiwa katika ukaribu kuvuja mtandaoni.
Tukio hilo lilitokea juzi ambapo inasemekana Prezzo alikuja Tanzania kwaajili ya kufanya kazi na msanii Dogo Janja.
Hizi ni baadhi ya picha zinazowaonyesha Prezzo na Amber lulu pamoja;


Katika kipindi cha XXL cha Clouds FM mtangazaji Soudy Brown aliwatafuta Prezzo na Amber lulu walifunguka yafuatayo;
“Nilivyojaribu kumchek kwa simu alipokea na sauti yake ilikuwa inasound kama katoka usingizini nikamuuliza uko wapi? akajibu yupo nyumbani kwa mbaalii nikasikia sauti ya Prezzo nikamuomba Amber lulu ampatie simu Prezzo na yeye alikuwa sound katoka kulala, Nikamuuliza vipi mzee baba umeingia lini Bongo? Akajibu yupo tangu jana, Nikamuuliza uko wapi akajibu yupo boardroom ya Seacliff hotel nikamwambia mbona nasikia mwangwi? Akajibu it’s true wako boardroom na Amber lulu ni rafiki yake na ndugu yake hawezi kumtamani”.
Prezzo alipoulizwa kama yupo tayari kumuita Jaquar Mheshimiwa Mbunge akajibu yeye ni president hawezi kumwita Mheshimiwa mbunge wake.