Pettit Man:Papii ni Ndugu Yangu Kabla Hajapata Matatizo.
Moja ya mameneja maarufu wa wasanii nchini , Pettit Man amefunguka na kuongelea mahusiano yake ya muda mrefu na wasani Papii kocha na baba yake Nguza Viking na kusema kuwa walikuwa marafiki na kama ndugu kwa muda mrefu kabla hata watu hao hawajapata matatizo na kuwekwa ndani kwa kipindi chote hicho.
Pettit Man anasema kuwa pamoja na kwamba hata yeye anafanya kazi ya kuwa-menage wasanii lakini haimaanishi kuwa karibu na papii kocha ina maana kuwa yeye ndio kiongozi wake ila tu ukaribu wake ndio unaomfanya kuwa nao karibu kila siku katika kazi zao.ika na nikawa naenda kuwaona
nina menejimenti yangu ndio,na mtarajie kuona wasanii wengi tu wazuri wakitoka lakini katika menejiment yangu wasanii papii na baba yake hawapo wao wana uongozi wao ili walikuwa wana nichukua kipindi hicho kipindi hicho wako T.O.T na kuniingiza kwenye muziki nikiwa bado mdogo.
matatioz yamewafika nikiwa nje ila nilifika na nikawa naenda kuwaona zaidi ya mara moja kwaio ni ndugu zangu tangu kabla hata hawajapata matatizo na hata sasa still ni ndugu zangu.
Kwa kuongezea hapo Pettit Man anasema kuwa kwa sasa wanatakiwa kushirikina na kuweka vitu vingine pembeni kwa kuwa wanahitaji sana msaada wao na kwa kuwa wamepitia matatizo makubwa sana wanahitaji kusaidiwa ili waweze kusahau matatizo yako.
Kwenye kaiz tunafanya kazi, atakaponihitaji na kuniita nimsaidie au anisaidie tutafanya kazi tu, kwa sababu tulishakuwa kama ndugu sasa ,unajua hakuwepo kwa muda mrefu sana kwaio inabidi tumsaidie ili arudi kwenye hali yake na pia aweze kusahau matatioz yake ya nyuma.