Penny Ategemea Ndoa Mwaka Huu
Mtangazaji maarufu wa luninga ya afrika magic swahili katika kipindi cha n harusi yetu amewapa moyo mashabiki wake na kuwaambia kuwa mwaka uliopita haukuwa mwaka mzuri sana kwake hasa katika swala la ndoa na mahusiano lakini sasa hivi wakae mkao wa kula kwa sababu bwana yuko tayari kwa ajili ya harusi,
Penny anasema kuwa mwaka 2017 ulikuwa ni mwaka wenye gundu kwake lakini anashukuru Mungu mwaka huo umepita na kwa mwaka huu anategemea kila kitu kitakuwa sawa na bwana harusi yuko tayari kwaiyo wategemee ndoa.
mwaka huu ni mwaka wa baraka kwangu na gundu nyingi zilizokuwepo zilishaondoka 2017,mwaka huu kwangu ni ishara na shela litakaa mwilini mwangu, bwana harusi yupo tayari kwa mwaka huu.
Hata hivyo Penny hakutaka kumsema mwanaume ambae yupo nae katika mahusiano ingawa amewathibitishia mashabiki kuwa ndo mwaka huu ni lazima.
Penny alishawahi kuwa katika mahusiano na msanii mkubwaTtanzania Diamond Platinumz na kupata mimba yake lakini aliitoa mimba hiyo na kusababisha mahusino yao kuvunjika.