Patrick Kanumba Akana Kuwa na Mapenzi Na Jennipher.
Ni zaidi ya miaka sita imepita tangu watoto wadogo waliotambulishwa kwenye game la bongo movies kuweza kusimamam wenyewe baada ya kifo cha aliyekuwa kama baba yao katika kazi za sanaa Steven Kanumba kufariki.watoto hao hivi karibuni waliingi katika skendo ya kuingia katika mahusiano ya kimapenzi .
Patrick na Jennipher ni vijana wadogo ambao bado wanakuzwa katika tasnia ya filamu nchini lakinin pia ni vijana wanaoonekana kuwa na vipaji ambao ndoto zao zilianza kukatika baada ya msanii aliyekuwa akiwasimamamia kwa karibu kauaga dunia.
Akiongea na waandishi wa habari Patrick Kanumba amekana tetesi hizo na kusema kuwa maneno hayo ni uongo mtupu na hakuna jambo kama hilo bali watu wamekuwa wakizusha tu,Patrick anasema kuwa maneno hayo ya uvumi amekuwa akiyasikia yakisemwa katika mitandao lakini ameamua kuyapuuzia kwa sababu hayana ukweli wowote.
Patrick anasema kuwa tangu wameazana kufanya kazi na Jennipher wao wameshakuwa kama ndugu kwa sababu wameweza kuziinganisha hadi familia zao na kuwa familia moja hivyo hawezi kufanya kitu kama hicho hata mara moja.