Otile Brown Akiri Kulikumbuka Penzi La Vera
Msanii wa muziki anayefanya vizuri nchini Kenya Otile Brown amefunguka na kukiri kumiss aliyekuwa mpenzi wake Socialite Maarufu Vera Sidika.
Otile alifunguka hayo Siku chache zilizopita ilipokuwa kumbu kumbu ya kuzaliwa kwa Vera Sidika.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Otile amemposti Vera na kumuandikia maneno mengi matamu huku akikiri kuwa Vera mkarimu na mtu mzuri na kuna wakati anakuwa anamkumbuka sana.
https://www.instagram.com/p/BoWPmfKny-T/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=buv5q7dlscik
Vera Sidika yupo Dubai ambako anakula bata la Birthday yake hivyo hajamjibu Ex wake huyo.
Vera na Otile Brown waliachana mapema mwezi uliopita baada ya kuwa Kwenye Mahusiano kwa Miezi kadhaa huku kila mmoja akimtuhumu mwenzake kama kuwa chanzo cha kuisha kwa Penzi lao.