Ommy Dimpoz Aibukia Nchini Kenya
Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz ameonekana nchini Kenya Baada ya kipindi cha muda kidogo ambacho hakuonekana.
Ommy Dimpoz amekuwa kimya kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii toka Decemba Mosi mwaka jana. Kuliibuka taarifa za yeye kuzidiwa na kupelekwa nchini Ujerumani kwaajili ya matibabu tena lakini taarifa hizo zilitupiliwa mbali na watu wake wa karibu.
Baada ya kimya kirefu Ommy Dimpoz ameonekana nchini Kenya akiwa na msanii wa Kenya anayejulikana Kama Willy Paul Msafi.
Willy Paul ameposti picha inayomuonyesha akiwa na Ommy Dimpoz katika ukurasa wake wa Instagram na kusindikiza kwa maneno yaliyosomeka “Happy to see my Brother”.
https://www.instagram.com/p/Bs5lkk6gEuB/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1n9rmz0yf9jxe
Ommy Dimpoz na Willy Paul wamekutana Kenya, bado haijajulikana iwapo wawili hao wamekutana kwa lengo la kudumisha urafiki au ni kazi pekee.