Odama Apata Kigugumizi Tetesi Za Ujauzito.
Kumekuwa na tetesi za muda mrefu kuhusu msanii wa bongo movie Tanzania kuwa ni mjamzito na kwamba aamekuwa akificha jambo hilo,hata hivyo msanii huyo alipoulizwa kuhusu swala hilo alijikuta akipatwa na kigugumizi na kushindwa kutoa tamko rasmi kuhusu swala hilo la yeye kuwa mjamzito .
Akiongea na star mix ya GPL,Odama kwa njia ya simu alisema kuwa kuhusu swala la yeye kuwa mjamzito ni swala nyeti sana, hawezi kuongelea swala hilo kwa sababu yuko mbali na nyumbani.Hata hivyo alimuomba mwandishi kuwa mvumilivu mpaka atakaporudi ndio waweze kuzungumzia swala hilo.
. Nipe muda nilitafakari swali lako, lakini kama hutojali tunaweza kuzungumza mambo mengi hilo naomba tuachane kabisa aidha unaweza kuningoja mpaka nirudi tuzungumze ana kwa ana kuhusu swala hilo kwa sasa wala hata siwezi kukwambia kama nina mimba au sina. -Alisema Odama kwa njia ya simu.
Wasanii wengi wa kike wamekuwa wakishindwa kusema mbele za watu au katika vyombo vya habari kuhusu swala la wao kuwa wajawazito ingawa kuwa mjamzito ni swala la kheri kwa kila mtu