Odama Akiri Kujitenga Mbali na Watu Wambea
Muigizaji wa Bongo movie Jennifer Kyaka maarufu kama Odama ameibuka na kuweka wazi kuwa anapenda kujitenga na kujiweka mbali na watu ambao wanafatilia maisha ya wengine.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Odama ameweka wazi kuwa ukurasa kufanikiwa kwenye maisha ya kufuata ya kwani na Ndio maana anapenda kuzungukwa na marafiki ambao sio wambea na wanaofanya yao.
Katika maisha yangu nawapenda sana watu ambao hawafuatilii mambo ya wengine, wako bize na yao, hata rafiki zangu wengi wako hivyo si watu wa mambo ya umbeyaumbeya“.
Mimi nikimuona mtu hafuatilii maisha ya mwingine nampenda sana na tena nampa heshima yake kubwa, kwa sababu najua anajielewa.
Kwangu mimi huyo anaweza hata kuwa rafiki yangu mkubwa, maana mtu ukiwa kila wakati unachunguza mambo ya mwenzako, yako utayafanya wakati gani?”.