Ochu Sheggy Akanusha Tetesi Za Kupigwa Na Mpenzi Wake
Kumekuwa na tetesi katika mitandao zinazodai kuwa msanii Ochu Sheggy ambae yupo katika mahusiano ya kimapenzi na msanii mwenzie Witnesss Kibonge Mwepesi, ambao wamedumu katika mahusiano kwa zaidi ya miaka mitano na kufanikiwa kupata mtoto mmoja kuwa na yeye pia ni moja ya wanaume ambao wanalelewa na mwanamke huyo na anapofanya kosa huwa anapokea kipondo toka kwa mama mzazi wa mtoto wake huyo.Tetesi hizo zinazotaka kumfananisha msanii Ochu na msanii wa Bongo fleva Nuh Mziwanda katika penzi lake la nyuma na msanii mwenzie Shiloleh ambapo inasemekana kuwa msanii huyo alikuwa akipokea kichapo cha nguvu kutoka kwa Shiloleh ana alikuwa hana sauti ya kusema kitu chochote kwa mwanamke wake.
Hata hivyo alipokuwa akiongea na eNews ya EATV, msanii Ochu Sheggy alikanusha uvumiwa tetesi hizo na kusema kuwa” watu wanakuwa wanatafsiri picha wanazoziona tofauti na vile uhalisia ulivyo, saa zingine watu picha wanayoiona sio vile picha ilivyo,jinsi mnavyomuona witness ni tofauti na mnavyomfikiria, ni mtu anayelainika mno,kama yeye ni chuma mimi ni greese, na kazi ya greese mnaijua kwenye chuma ni kulainisha chuma kiweze kufanya kazi vizuri,” alifunguka Ochu Sheggy
Hata alipoulizwa kuhusu kujitetea huko ikiwa kama njia ya kutotaka kujiaibisha msanii Ochu alisema kuwa kwake yeye ni mwiko mtoto wa kike kumpiga na hawezi kupigwa na mkewe”kwangu ni mwiko kwa mtoto wa kike yeyote yule kunipiga na haitawahi kutokea,na wapo wanaosema yeye ni mgumu ila huo ugumu wake mimi sijawahi kuuona, tje more wanavyomuona mgumu ndio mimi namuona yuko sex.” Aliongezea Ochu
Hata hivyo, katika kuendelea kujitetea Ochu Sheggy alisema kuwa watu wanaosema Witness hapiki , na mwanaume huyo muda mwingi anaonekana katika vibanda vya chipsi,alisema kuwa kwa muda mwingine inakuwa vigumu kupika usiku ilhali wao wote ni wasanii na wanakuwa wanabanwa na kazi za muziki hivyo inabidi wasaidiane katika ilo.
Kwa muda mrefu Witness na Ochu wamekuwa ni moja ya wasanii waliopo katika mahusiano lakini hawajawahi kupata skendo mbaya yeyote, hii inaweza kuwa ni mara ya kwanza watu kumzushia maneneo hayo