“Nyimbo Zangu Kufungiwa Hakunipunguzii Kitu”-Diamond Platnumz
Mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz anayefanya vizuri na albamu yake mpya ya ‘A boy from Tandale’ amefunguka na kudai kufungiwa kwa nyimbo zake mbili hakumpunguzii kitu.
Wiki chache zilizopita BASATA ilifungia nyimbo kumi na tano za wasanii mbali mbali wa Bongo fleva kwa kudai zimekiuka maadili ya Kitanzania na moja ya wasanii hao ni Diamond ambaye alifungiwa nyimbo mbili Wakawaka na Halelujah.
Kwenye Interview aliyofanya na The Playlist ya Times Fm Diamond amefunguka na kudai yeye kufungiwa nyimbo zake hakumpunguzii kitu zaidi ni kama kumkomoa na kurudisha nyuma jitihada za kukuza mziki huu wa Bongo fleva.
Suala si kufungia tu nyimbo, mimi ukinifungia nyimbo hainipunguzii kitu nikienda nje naenda nai-perform ukiwa hutaki sinaondoka tu naenda nchi nyingine, kwa hiyo ni kukaa tuzungumze, tuelekezane lakini tusifanye kama kukomoana, hapana, tufanye katika mazingira ambayo yatasaidia sanaa ikue“.
Bongo Flava naijua kweli kweli, halafu kama mimi ni mtu ambaye siogopi kwenda jela kwa ajili ya Bongo Flava, siogopi kufanya chochote kwa sababu ndio Baba yangu na Mama yangu ndio nimefanya hadi nimefika hapa, kwa hiyo unapo-deal na sanaa yangu hakikisha unafanya kitu ambacho kipo sahihi usikurupuke kwa sababu una mamlaka”.
Diamond pia amesema hivi sasa jitihada zake anazielekeza kwenye uzinduzi wa radio station na television station zake za Wasafi TV na Wasafi Radio pamoja na kuhakikisha albamu yake inafanya vizuri sokoni.