Nyimbo za Diamond Zilizofungiwa Zazua Gumzo Bungeni
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) kupitia Vijana Mkoa wa Arusha, Catherine Magige amehoji sababu ya kufungia nyimbo za Mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz kwa kigezo cha kukosa maadili baada ya kuziacha zikachezwa kwa muda mrefu hewani.
Wiki chache zilizopita BASATA lilitangaza kufungia nyimbo zaidi ya kumi na tano za wasanii mbali mbali na mmoja ya wasanii aliyefungiwa nyimbo zake ni Diamond Platnumz ambapo alifunguwa nyimbo mbili kwa kigezo cha Kukiuka maadili ya Kitanzania.
Akijibu swali hilo, Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, amejibu kuwa Diamond siyo msanii wa kwanza kufungiwa nyimbo zake kwani hata wasanii wa Nigeria, Davido na Wizkid, wamefungiwa nyimbo zao. Pia alimtaja mwanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasiaya Congo, Kofii Olomide, ambaye wimbo wake wa Ekoti Te umefungiwa nchini humo.
Pamoja na kuibuka wabunge wengi wenye kutaka kutoa taarifa na kuendelea hoja hiyo, Naibu Spika, Tulia Ackson, hakuwapa nafasi.